Hello, leo
nitawaonesha jinsi ya kuhifadhi/ficha vitu vyako kwenye GOOGLE DRIVE kwenye simu yako.
KWA UFUPI
GOOGLE
DRIVE ni huduma ya uhifadhi wa faili na maingiliano iliyoundwa na Google.
Ilizinduliwa Aprili 24, 2012, Hifadhi ya Google inaruhusu watumiaji kuhifadhi
faili kwenye seva zao, kwa upande
wa simu inaweza
tumika kwenye simu
aina ya Android na iOS unaweza tumia
kuhifadhi vitu mbalimbali
zenye format aina
zote (MFANO picha, video. Pdf,
ms, software, vyeti, hati za nyumba na vituvingine vyovyote ambavyo ni private).
GOOGLE
DRIVE hutoa gigabytes 15 za uhifadhi wa
bure kupitia Google One. Google One pia hutoa gigabytes 100, gigabytes 200,
terabytes 2, terabytes 10, terabytes 20, na terabytes 30 zinazotolewa kupitia
mipango ya kulipwa kwa hiari. Faili zilizopakiwa zinaweza kuwa ukubwa wa hadi 5
terabyites kwa ukubwa.
JINSI YA
KUTUMIA
Unachotakiwa kufanya ni kufuata hizi
hatua zifuatazo:
HATUA YA
KWANZA
Nenda kwenye
menyu ya simu
yako ufungue DRIVE,
Kama haipo inabidi
ui-install kwenye google
play store.
HATUA YA PILI
Itafunguka Hivi kama uonvyo hapo chini
HATUA YA TATU
Hakikisha email yako inasoma kwenye DRIVE kama hakuna angalia duara mkono wa kushoto kisha ubonyeze kuhakiki au angalia mkono wa kulia uangalie kama itaonekana picha uliyosave kwenye profile ya email yako au herufi ya jina lako.
HATUA YA NNE
Hakiki storage yako, kumbuka google wanakupa GB15 za kutumia bure, ukitaka kuongeza zaidi inabidi ulipie ila so far hakuna mtu anayezifkia hizo kwa matumizi ya simu.
HATUA YA TANO
JINSI YA KU-UPLOAD KITU KWENYE DRIVE, bonyeza ala ya kujumlisha (ili kuadd ADD)
HATUA YA SITA
Baada ya kubonyeza + zitatoka option tofauti zote ni muhimu ila leo tunaangalia jinsi ya ku-upload kitu ambacho tiyali kipo kwenye simu, hivyo ili kuingiza na kuhifadhi inabidi ubonyeze upload (option iliyozungushiwa duara hapo chini)
HATUA YA SABA
Itakupeleka kwenye vitu ambavyo umetumia muda sio mrefu (RECENT) kama picha unayotaka kuiupload haionekani hapa unatakiwa kubonyeza hilo duara mkono wa kushoto pembeni mwa neno RECENT.
HATUA YA NANE
Itakupeleka kwenye source ya mafaili yako kila simu ipo tofauti ila baadhi ya vitu vipo sawa so, mfano unataka kuupload picha. Unakwenda kwenye
IMAGES
HATUA YA TISA
Picha ninayotaka kui-upload ipo kwenye folder la bluetooth
HATUA YA KUMI
Chagua picha utakayo
HATUA
YA KUMI NA MOJA
Ukiipata
ibonyeze kwa nguvu mpaka itokee tiki then
nenda kulia kwako utaona neno OPEN ibonyeze ili
ianze ku-up-load
HATUA
YA KUMI NA MOJA
Baada
ya kuopen Itatokea hivi, bonyeza ALLOW ili
kuruhusu DRIVE kupata access ya mafaili
ya simu yako
HATUA
YA KUMI NA MBILI
Baada
ya hapo itaanza ku-upload. MUHIMU kila
simu inasetting tofauti so inategemea simu
yako umeiset vipi kwenye network, simu
nyingine zina-upload moja kwa moja nyingine mpaka
ubonyeze neno RESUME kama ionekanavyo
hapo chini.
HATUA
YA KUMI NA TATU
Baada
ya hatua ya 12 kukamilika picha yako
itaupload kwenye DRIVE. Hivyo
unamaamuzi ya kuifuta picha original
iliyopo kwenye simu au kuicha kwani
ikiwa kwenye DRIVE inakaa huko
mpaka utakapo amua wewe kuifuta
NJIA
YA PILI YA JINSI YA KUHIFADHI AU
KUFICHA VITU KWAKO KWENYE GMAIL
1.
FUNGUA GALLARY AU GOOGLE PHOTOS
chagua picha utakayo kuiweka kwenye
GOOGLE DRIVE ibonyeze kwa nguvu then
share kwenye Drive (fanya kama
unavyofanya unapomrushia mtu kitu kwenye
Bluetooth )
2.
CHAGUA KUSHARE KWENYE DRIVE kama ioneshavyo
hapo chini
3.
ITAFUNGUKA HIVI utaamua wewe mwenyewe kuirename
au kuiacha kama ilivyo kisha
bonyeza SAVE
4.
ITAFUNGUKA HIVI UTABONYEZA RESUME
5.
UNAKUA UMEMALIZA THEN ITAANZA KU-UPLOAD
6.
IKIMALIZA KULOAD PICHA INAKUA IMEKAA KWENYE DRIVE
DONE
Hatua hizi
unaweza zifanya kwa mafaili ya aina
yote utakayo na yanakua salama so hata
ikitokea umepoteza simu yako au umepoteza hard
copy ya vitu vyako bado unakua na
backup ya data zako muhimu kwenye
DRIVE bila tatizo lolote