Hi my name is Gualbert F.Kashasha, and I have a lot to share with you, a year ago I created this blog in order to share with you all my stories & all my adventures with you, my dear friend. You might find it sad, amusing or horrifying. But I hope we’ll ride together all the way.
Friday, October 16, 2020
JINSI YA KUKABILIANA NA BLACKMAILER (HOW TO DEAL WITH A BLACKMAILER)
This summary is not available. Please
click here to view the post.
Saturday, July 18, 2020
JINSI YA KUHIFADHI VITU VYAKO KWENYE GOOGLE DRIVE
Hello, leo
nitawaonesha jinsi ya kuhifadhi/ficha vitu vyako kwenye GOOGLE DRIVE kwenye simu yako.
KWA UFUPI
GOOGLE
DRIVE ni huduma ya uhifadhi wa faili na maingiliano iliyoundwa na Google.
Ilizinduliwa Aprili 24, 2012, Hifadhi ya Google inaruhusu watumiaji kuhifadhi
faili kwenye seva zao, kwa upande
wa simu inaweza
tumika kwenye simu
aina ya Android na iOS unaweza tumia
kuhifadhi vitu mbalimbali
zenye format aina
zote (MFANO picha, video. Pdf,
ms, software, vyeti, hati za nyumba na vituvingine vyovyote ambavyo ni private).
GOOGLE
DRIVE hutoa gigabytes 15 za uhifadhi wa
bure kupitia Google One. Google One pia hutoa gigabytes 100, gigabytes 200,
terabytes 2, terabytes 10, terabytes 20, na terabytes 30 zinazotolewa kupitia
mipango ya kulipwa kwa hiari. Faili zilizopakiwa zinaweza kuwa ukubwa wa hadi 5
terabyites kwa ukubwa.
JINSI YA
KUTUMIA
Unachotakiwa kufanya ni kufuata hizi
hatua zifuatazo:
HATUA YA
KWANZA
Nenda kwenye
menyu ya simu
yako ufungue DRIVE,
Kama haipo inabidi
ui-install kwenye google
play store.
HATUA YA PILI
Itafunguka Hivi kama uonvyo hapo chini
HATUA YA TATU
Hakikisha email yako inasoma kwenye DRIVE kama hakuna angalia duara mkono wa kushoto kisha ubonyeze kuhakiki au angalia mkono wa kulia uangalie kama itaonekana picha uliyosave kwenye profile ya email yako au herufi ya jina lako.
HATUA YA NNE
Hakiki storage yako, kumbuka google wanakupa GB15 za kutumia bure, ukitaka kuongeza zaidi inabidi ulipie ila so far hakuna mtu anayezifkia hizo kwa matumizi ya simu.
HATUA YA TANO
JINSI YA KU-UPLOAD KITU KWENYE DRIVE, bonyeza ala ya kujumlisha (ili kuadd ADD)
HATUA YA SITA
Baada ya kubonyeza + zitatoka option tofauti zote ni muhimu ila leo tunaangalia jinsi ya ku-upload kitu ambacho tiyali kipo kwenye simu, hivyo ili kuingiza na kuhifadhi inabidi ubonyeze upload (option iliyozungushiwa duara hapo chini)
Itakupeleka kwenye vitu ambavyo umetumia muda sio mrefu (RECENT) kama picha unayotaka kuiupload haionekani hapa unatakiwa kubonyeza hilo duara mkono wa kushoto pembeni mwa neno RECENT.
HATUA YA NANE
Itakupeleka kwenye source ya mafaili yako kila simu ipo tofauti ila baadhi ya vitu vipo sawa so, mfano unataka kuupload picha. Unakwenda kwenye IMAGES
HATUA YA TISA
Picha ninayotaka kui-upload ipo kwenye folder la bluetooth
HATUA YA KUMI
Chagua picha utakayo
HATUA
YA KUMI NA MOJA
Ukiipata
ibonyeze kwa nguvu mpaka itokee tiki then
nenda kulia kwako utaona neno OPEN ibonyeze ili
ianze ku-up-load
HATUA
YA KUMI NA MOJA
Baada
ya kuopen Itatokea hivi, bonyeza ALLOW ili
kuruhusu DRIVE kupata access ya mafaili
ya simu yako
HATUA
YA KUMI NA MBILI
Baada
ya hapo itaanza ku-upload. MUHIMU kila
simu inasetting tofauti so inategemea simu
yako umeiset vipi kwenye network, simu
nyingine zina-upload moja kwa moja nyingine mpaka
ubonyeze neno RESUME kama ionekanavyo
hapo chini.
HATUA
YA KUMI NA TATU
Baada
ya hatua ya 12 kukamilika picha yako
itaupload kwenye DRIVE. Hivyo
unamaamuzi ya kuifuta picha original
iliyopo kwenye simu au kuicha kwani
ikiwa kwenye DRIVE inakaa huko
mpaka utakapo amua wewe kuifuta
NJIA YA PILI YA JINSI YA KUHIFADHI AU KUFICHA VITU KWAKO KWENYE GMAIL
1.
FUNGUA GALLARY AU GOOGLE PHOTOS
chagua picha utakayo kuiweka kwenye
GOOGLE DRIVE ibonyeze kwa nguvu then
share kwenye Drive (fanya kama
unavyofanya unapomrushia mtu kitu kwenye
Bluetooth )
2.
CHAGUA KUSHARE KWENYE DRIVE kama ioneshavyo
hapo chini
3.
ITAFUNGUKA HIVI utaamua wewe mwenyewe kuirename
au kuiacha kama ilivyo kisha
bonyeza SAVE
4.
ITAFUNGUKA HIVI UTABONYEZA RESUME
5.
UNAKUA UMEMALIZA THEN ITAANZA KU-UPLOAD
6.
IKIMALIZA KULOAD PICHA INAKUA IMEKAA KWENYE DRIVE
DONE
Hatua hizi
unaweza zifanya kwa mafaili ya aina
yote utakayo na yanakua salama so hata
ikitokea umepoteza simu yako au umepoteza hard
copy ya vitu vyako bado unakua na
backup ya data zako muhimu kwenye
DRIVE bila tatizo lolote
Tuesday, June 9, 2020
MARRY’S FORGIVENESS pt1
JE WEWE UNGEFANYA NINI?
Mzee John Charles Kayumba alibarikiwa na Mungu, ujanani mwake Mungu alimbariki akapata mke mwema aitwaye Rose Jamini , wote walikuwa ni wachamungu, kama walivyo wanandoa wengine wa zamani walipitia mengi katika maisha yao ya ndoa shida na raha, lakini walivumilia na mpaka Mungu akawajalia kupata watoto wanne, wakiume watatu na msichana mmoja. (Charles, Emilianna, Makuda na Mussa). Mzee huyo alikuwa ni mtumishi serikalini na mkewe huyo alikuwa ni mama wa nyumbani anayeendesha biashara ndogondogo. Maisha yaliendelea, walilea watoto wao na kuishi kwa furaha sana. Miaka ilipita wakabarikiwa kujenga nyumba tatu, ambapo nyumba moja waliishi wao na watoto wao na nyingine walipangisha.
Siku moja ilikuja kugundulika kuwa mzee huyo alizaa mtoto mwingine nje ya ndoa. Mkewe alihuzunika na kuumia sana, Baada ya mkewe kupata habari hizo kutoka kwa majirani, alifanya uchunguzi na kugundua kuwa habari hizo ni za kweli, na nikweli mzee huyo alizaa mtoto wa kike na mwanamke mwingine. Siku moja baada ya kupata na kukamilisha upelelezi wake na kupata uhakika alimsubiri mumewe na kumuuliza, Mumewe alikiri na kukubali jambo hilo. Jambo hilo lilileta mvurugano kwenye ndoa yao kiasi kwamba ililazimu kuitwa wazazi na ndugu wa pande zote mbili pamoja na viongozi kathaa wa dini ili waje kulisuluhuisha, kikao kilikua kikubwa na kirefu sana ila Mungu ni mkubwa, maana aliwezesha usuluhuisho huo kuwa wa amani na Yule mke kumsamehe mumewe, wageni walioalikwa kwenye kikao hicho waliamuru mume arudi kwenye ndoa na aachane na huyo mwanamke mwingine.
Miezi kadhaa ilipita mke wa Mzee John alimuomba mumewe amlete huyo mtoto aje kukaa nyumbani kwao na kumlea pamoja na wenzake, mzee John alifurahi sana kwani aliona ni jambo bora watoto wake wakikua pamoja wakitambuana na kupendana kama ndugu. Kweli Yule mtoto alikuja nyumbani hapo na kulelewa na mama huyo, Alikua anaitwa Mary, alisomeshwa na kuishi hapo kipindi chote hadi alipomwaliza shule ya msingi, Mungu alimjalia kwani alifaulu mtiani wake na kuendelea na elimu ya sekondali. Kipindi yupo kidato cha pili Mzee John (baba yake) alifariki. Ilikua ni pigo kubwa kwenye familia hiyo, mazishi yalifanyika. Ilipofika siku ya mirathi Mama na Ndugu zake Mary ( dada na kaka zake pamoja na mama yake aliyekuwa anamlea ) walimkataa na kumwambia kuwa hawamtambui, mama mjane alitoa maelezo kwenye kikao hicho kuwa binti huyo alikua ni mfanyakazi wao wa ndani na waliamua kumlea na kumsomesha kama mwanafamiia ila sio mtoto halali wa mwarehemu mumewe na inatakiwa aondoke arudi kwao, Binti Yule hakuamini kinachomtoka kinywani mama yake huyo aliangua kilio na kuuliza kama kunakitu amekosea hadi leo amkatae, alihuzunika sana na kuamua kuondoka na kurudi kwa mama yake mzazi.
Maisha ya mama yake yalikua ya kimaskini sana. Alimpokea mwanae na kuishinae hapo. Ingawa alikua bado anasoma hakuwa na budi kumsaidia mama yake baadhi ya shughuli ili waweze kupata kipato, siku za kawaida baada ya kurudi shule alikua anakwenda mgahawani kwa mama yake na kumsaidia kazi, alipata usumbufu mwingi kutoka kwa wateja wa kiume ambao mara nyingi walikua wakimtongoza na kumtaka kimapenzi. Kutokana na malezi aliyopewe na heshima aliliokuwa nayo alijitahidi kudharau usumbufu huo ila ulivyoukua unazidi alibidi awe mkali. Mama yake alimsihi asiwe mkali kwa wateja kwani akifanya hivyo watamkimbia mgahawani kwake na ukiangalia tangu yeye arudi wateja wamekua wengi, alimwambia anachotakiwa kufanya ni kuwasikiliza ila asifanye au kukubali watakavyo. Alifanya hiyo ila kadri siku ziendavyo vishawishi vilizidi kuwa vingi shuleni na nyumbani, kwani hata baadhi ya waalimu nao walikua wanamtaka. Akajikuta anahongwa na wateja, wengine kumuachia hela kubwa wakidai ni zawadi. Mary aliangalia maisha ya marafiki zake shuleni wengi wanavaa vizuri na wengine wanamiliki hadi simu. Mary bado akapiga moyo konde na kubaki kwenye mstari.
Siku moja wakati anatoka shule alisikia mlio wa honi ya pikipiki, alipogeuka nyuma alikuta ni teacher wake, teacher alimuomba ampe lifti Mary hakua na shaka kwakua alijua mwalimu anapitaga njia moja ya nyumbani kwao, alipanda pikipiki huku teacher akimpa pole kwa kutembea umbali mrefu. Njiani teacher alimuomba apitie nyumbani kwake kwanza abadili nguo kisha ampeleke mpaka kwao. Mary alikubali, walipofika nyumbani kwa teacher mary alibaki nje Teacher akaingia ndani kubadili nguo, kipindi yupo nje alishangaa anaitwa na teacher aingie ndani, mary alijibu hawezi kwani anaharaka kurudi akamsaidie mama yake, Teacher aliendelea kumuomba aingie ili amsaidie kusahihisha mitihani, Mary aliomba aende anaogopa mama atamgomba kama akichelewa, Teacher alimwambia anamitihani michache tu hivyo amsaidie fasta ili amuwahishe, Mary alimuomba basi aitoe nje ila teacher akamwambia nje watu wakiona watahisi vibaya. Basi Mary akajikuata anakubali, aliingia ndani na kukuta mitihani ipo mezani marry alikaribishwa kwenye kochi akaaanza kusahisha,

End of part
one
Subscribe to:
Posts (Atom)
MASWALI YANAYOWEZA KUULIZWA KWENYE INTERVIEW YA TRA MARCH 2025
ANGALIZO Haya ni baadhi ya mawaswali ambayo yanaweza yakatoka au yasitoke kutokana na ajira ulioiomba, hiyo unatakiwa kuyapitia na kuso...
-
H ello, leo nitawaonesha jinsi ya kuhifadhi/ficha vitu vyako kwenye GOOGLE DRIVE kwenye simu yako. KWA UFUPI GOOGLE DRIVE ni...
-
“Unaweza kumnunua binadamu lakini uwezi kummiliki binadamu” “ Umekuja duniani peke yako, na utaon...