Tuesday, June 9, 2020

MARRY’S FORGIVENESS pt1



JE WEWE UNGEFANYA NINI?
       Mzee  John Charles Kayumba  alibarikiwa  na Mungu, ujanani mwake Mungu alimbariki akapata mke mwema  aitwaye Rose Jamini , wote walikuwa ni wachamungu, kama walivyo wanandoa wengine wa zamani walipitia mengi katika maisha yao ya ndoa shida na raha, lakini walivumilia na mpaka Mungu akawajalia kupata watoto wanne, wakiume  watatu na msichana mmoja. (Charles, Emilianna, Makuda na Mussa). Mzee huyo alikuwa ni mtumishi serikalini na mkewe huyo alikuwa ni mama wa nyumbani anayeendesha biashara ndogondogo. Maisha yaliendelea, walilea watoto wao na kuishi kwa furaha sana. Miaka ilipita wakabarikiwa kujenga nyumba tatu, ambapo nyumba moja waliishi wao na watoto wao na nyingine walipangisha.

          Siku moja ilikuja kugundulika kuwa mzee huyo alizaa mtoto mwingine nje ya ndoa. Mkewe alihuzunika na kuumia sana, Baada ya mkewe kupata habari hizo kutoka kwa majirani, alifanya uchunguzi na kugundua kuwa habari hizo ni za kweli, na nikweli mzee huyo alizaa mtoto wa kike na mwanamke mwingine. Siku  moja  baada  ya  kupata  na  kukamilisha  upelelezi wake na kupata uhakika alimsubiri mumewe na kumuuliza, Mumewe alikiri na kukubali jambo hilo. Jambo hilo lilileta mvurugano kwenye ndoa yao kiasi kwamba ililazimu kuitwa wazazi na  ndugu  wa pande zote mbili pamoja na viongozi  kathaa wa dini ili waje kulisuluhuisha, kikao  kilikua  kikubwa na kirefu sana  ila  Mungu ni mkubwa, maana aliwezesha usuluhuisho huo kuwa wa amani na Yule mke kumsamehe mumewe,  wageni walioalikwa kwenye kikao hicho waliamuru  mume arudi kwenye ndoa na aachane na huyo mwanamke mwingine.

        Miezi kadhaa ilipita mke wa  Mzee John alimuomba mumewe amlete huyo mtoto aje kukaa nyumbani kwao na kumlea pamoja na wenzake, mzee John alifurahi sana kwani aliona ni jambo bora watoto wake wakikua pamoja wakitambuana na kupendana kama ndugu.  Kweli Yule mtoto alikuja nyumbani hapo na kulelewa na mama huyo, Alikua anaitwa Mary, alisomeshwa na kuishi hapo kipindi chote hadi alipomwaliza shule ya msingi, Mungu alimjalia kwani alifaulu mtiani wake na kuendelea na elimu ya sekondali. Kipindi yupo kidato cha pili Mzee John (baba yake) alifariki. Ilikua  ni  pigo  kubwa  kwenye  familia  hiyo, mazishi  yalifanyika. Ilipofika siku ya mirathi Mama na Ndugu zake Mary ( dada na kaka zake pamoja na mama yake aliyekuwa anamlea ) walimkataa na kumwambia kuwa hawamtambui, mama  mjane alitoa  maelezo kwenye kikao hicho kuwa binti huyo alikua ni  mfanyakazi wao wa ndani na waliamua kumlea na kumsomesha kama mwanafamiia ila sio mtoto halali wa mwarehemu mumewe na inatakiwa aondoke arudi kwao, Binti Yule hakuamini kinachomtoka  kinywani mama yake huyo aliangua kilio na kuuliza kama kunakitu amekosea hadi leo amkatae, alihuzunika sana na kuamua kuondoka na kurudi kwa mama yake mzazi.

      Maisha  ya  mama  yake  yalikua  ya  kimaskini  sana. Alimpokea  mwanae na  kuishinae  hapo.  Ingawa  alikua  bado  anasoma  hakuwa na budi kumsaidia  mama yake  baadhi  ya  shughuli  ili waweze kupata  kipato,  siku za kawaida baada ya kurudi  shule alikua anakwenda mgahawani kwa  mama  yake  na  kumsaidia  kazi,  alipata  usumbufu  mwingi  kutoka  kwa  wateja  wa  kiume  ambao  mara  nyingi  walikua  wakimtongoza  na  kumtaka  kimapenzi. Kutokana na malezi  aliyopewe na heshima aliliokuwa nayo  alijitahidi  kudharau usumbufu  huo  ila  ulivyoukua unazidi alibidi awe mkali.  Mama  yake  alimsihi  asiwe mkali kwa wateja  kwani  akifanya  hivyo  watamkimbia  mgahawani  kwake  na  ukiangalia  tangu  yeye  arudi  wateja  wamekua  wengi,  alimwambia  anachotakiwa  kufanya  ni  kuwasikiliza  ila  asifanye  au  kukubali  watakavyo.  Alifanya  hiyo  ila  kadri  siku  ziendavyo  vishawishi  vilizidi  kuwa  vingi  shuleni  na  nyumbani, kwani  hata  baadhi  ya  waalimu  nao  walikua  wanamtaka.  Akajikuta  anahongwa  na  wateja,  wengine  kumuachia  hela  kubwa  wakidai  ni  zawadi.  Mary aliangalia  maisha ya marafiki zake shuleni  wengi  wanavaa vizuri na  wengine wanamiliki  hadi  simu.  Mary  bado  akapiga  moyo  konde  na  kubaki  kwenye  mstari.

     Siku  moja  wakati  anatoka  shule  alisikia  mlio  wa  honi  ya  pikipiki,  alipogeuka  nyuma  alikuta  ni  teacher  wake,  teacher  alimuomba  ampe  lifti  Mary hakua  na  shaka  kwakua  alijua  mwalimu  anapitaga  njia  moja  ya  nyumbani  kwao,  alipanda  pikipiki  huku  teacher  akimpa  pole  kwa  kutembea  umbali  mrefu.  Njiani  teacher  alimuomba  apitie  nyumbani  kwake  kwanza abadili  nguo  kisha  ampeleke  mpaka  kwao.  Mary  alikubali,  walipofika  nyumbani  kwa  teacher  mary  alibaki  nje  Teacher  akaingia  ndani kubadili  nguo,  kipindi  yupo  nje  alishangaa  anaitwa  na  teacher  aingie  ndani,  mary  alijibu  hawezi  kwani  anaharaka  kurudi  akamsaidie  mama  yake,  Teacher aliendelea  kumuomba  aingie  ili  amsaidie  kusahihisha  mitihani, Mary  aliomba aende anaogopa  mama  atamgomba  kama  akichelewa, Teacher  alimwambia anamitihani michache tu hivyo amsaidie fasta ili amuwahishe, Mary alimuomba basi aitoe nje ila teacher  akamwambia  nje  watu wakiona  watahisi  vibaya.  Basi  Mary  akajikuata  anakubali,  aliingia  ndani  na  kukuta  mitihani  ipo  mezani  marry  alikaribishwa  kwenye  kochi  akaaanza  kusahisha,
 End  of  part  one

NEW SERVICE ONLINE COMING SOON

Hello  guys,  we  are  happily  to  inform  you  that  our  blog  will  launch  new  online  services soon,  O'levelA'lever and  Collage  students  will benefit  from  this  new  project  as  well  as  other  individuals. 
I  know  the  feeling,  standing  in line  waiting  for  your  turn  to  come  up  while  fighting  the  deadline.  But  with  us  you  don't  have  to  worry,  because  now  you  don't  have  to   spend  more  time  in  stationery  waiting  for  the line  to  end.  just  Contact  us  and  we  do  your  work  in  minutes.

MASWALI YANAYOWEZA KUULIZWA KWENYE INTERVIEW YA TRA MARCH 2025

  ANGALIZO Haya ni baadhi ya mawaswali  ambayo yanaweza yakatoka au yasitoke kutokana na ajira ulioiomba, hiyo unatakiwa kuyapitia na kuso...