Saturday, July 18, 2020

JINSI YA KUHIFADHI VITU VYAKO KWENYE GOOGLE DRIVE


Hello, leo  nitawaonesha jinsi ya kuhifadhi/ficha vitu vyako kwenye GOOGLE DRIVE kwenye simu yako. 

KWA  UFUPI
GOOGLE DRIVE ni huduma ya uhifadhi wa faili na maingiliano iliyoundwa na Google. Ilizinduliwa Aprili 24, 2012, Hifadhi ya Google inaruhusu watumiaji kuhifadhi faili kwenye seva zao,  kwa  upande  wa  simu  inaweza  tumika  kwenye  simu  aina  ya  Android na iOS unaweza  tumia  kuhifadhi  vitu  mbalimbali  zenye  format  aina  zote  (MFANO picha, video. Pdf, ms, software, vyeti, hati za nyumba na vituvingine vyovyote ambavyo ni private). 

GOOGLE DRIVE  hutoa gigabytes 15 za uhifadhi wa bure kupitia Google One. Google One pia hutoa gigabytes 100, gigabytes 200, terabytes 2, terabytes 10, terabytes 20, na terabytes 30 zinazotolewa kupitia mipango ya kulipwa kwa hiari. Faili zilizopakiwa zinaweza kuwa ukubwa wa hadi 5 terabyites kwa ukubwa.

JINSI YA KUTUMIA
Unachotakiwa  kufanya  ni  kufuata  hizi  hatua  zifuatazo:

HATUA  YA  KWANZA
Nenda  kwenye  menyu  ya  simu  yako  ufungue  DRIVE,  Kama  haipo  inabidi  ui-install  kwenye  google  play  store.



HATUA YA  PILI
Itafunguka  Hivi  kama uonvyo hapo chini

HATUA  YA  TATU
Hakikisha  email  yako  inasoma kwenye DRIVE kama  hakuna  angalia  duara  mkono  wa  kushoto  kisha ubonyeze kuhakiki au  angalia  mkono  wa  kulia  uangalie  kama  itaonekana  picha  uliyosave  kwenye  profile  ya  email  yako  au  herufi  ya  jina  lako.




HATUA  YA  NNE
Hakiki  storage  yako,  kumbuka  google  wanakupa  GB15  za  kutumia  bure,  ukitaka  kuongeza  zaidi  inabidi  ulipie  ila  so  far  hakuna  mtu  anayezifkia  hizo  kwa  matumizi  ya  simu. 



HATUA  YA  TANO
JINSI  YA  KU-UPLOAD  KITU  KWENYE  DRIVE, bonyeza  ala  ya  kujumlisha (ili kuadd ADD)



HATUA YA SITA
Baada  ya  kubonyeza  +  zitatoka option  tofauti  zote ni muhimu ila leo  tunaangalia jinsi ya ku-upload kitu  ambacho  tiyali  kipo  kwenye  simu,  hivyo  ili  kuingiza na kuhifadhi inabidi  ubonyeze  upload (option iliyozungushiwa  duara hapo chini)



 HATUA YA SABA
Itakupeleka  kwenye  vitu  ambavyo  umetumia muda sio  mrefu  (RECENT) kama  picha  unayotaka  kuiupload  haionekani  hapa  unatakiwa  kubonyeza  hilo  duara  mkono  wa  kushoto  pembeni mwa  neno RECENT.

HATUA YA NANE
Itakupeleka  kwenye  source  ya  mafaili  yako  kila  simu  ipo  tofauti  ila  baadhi  ya  vitu  vipo  sawa  so,  mfano  unataka  kuupload  picha.  Unakwenda  kwenye  IMAGES


HATUA  YA  TISA
Picha  ninayotaka  kui-upload  ipo  kwenye  folder la bluetooth


HATUA  YA  KUMI
Chagua  picha utakayo





HATUA YA  KUMI NA MOJA
Ukiipata  ibonyeze  kwa  nguvu  mpaka  itokee  tiki  then nenda  kulia  kwako utaona neno  OPEN ibonyeze  ili  ianze  ku-up-load





HATUA YA KUMI NA MOJA
Baada  ya  kuopen Itatokea  hivi, bonyeza  ALLOW  ili  kuruhusu  DRIVE  kupata  access  ya  mafaili  ya  simu  yako






HATUA  YA  KUMI  NA  MBILI

Baada  ya  hapo  itaanza  ku-upload.  MUHIMU kila  simu  inasetting  tofauti  so  inategemea  simu  yako  umeiset  vipi  kwenye  network,  simu  nyingine  zina-upload  moja  kwa moja  nyingine  mpaka  ubonyeze  neno  RESUME  kama  ionekanavyo  hapo  chini. 



HATUA  YA  KUMI  NA  TATU
Baada  ya  hatua  ya  12  kukamilika  picha  yako  itaupload  kwenye  DRIVE.  Hivyo  unamaamuzi  ya  kuifuta  picha  original  iliyopo  kwenye  simu  au  kuicha  kwani  ikiwa  kwenye  DRIVE  inakaa  huko  mpaka  utakapo  amua  wewe  kuifuta 







NJIA  YA  PILI  YA  JINSI  YA  KUHIFADHI  AU  KUFICHA  VITU  KWAKO  KWENYE  GMAIL 


1.  FUNGUA  GALLARY  AU  GOOGLE PHOTOS
     chagua  picha  utakayo  kuiweka  kwenye  GOOGLE DRIVE ibonyeze  kwa  nguvu  then           share  kwenye  Drive (fanya  kama  unavyofanya  unapomrushia  mtu  kitu  kwenye                     Bluetooth  )


2. CHAGUA  KUSHARE  KWENYE  DRIVE  kama ioneshavyo  hapo  chini



3. ITAFUNGUKA  HIVI utaamua  wewe  mwenyewe  kuirename  au  kuiacha  kama  ilivyo  kisha          bonyeza  SAVE




4. ITAFUNGUKA  HIVI  UTABONYEZA  RESUME



5. UNAKUA  UMEMALIZA  THEN  ITAANZA  KU-UPLOAD



6. IKIMALIZA  KULOAD  PICHA  INAKUA  IMEKAA  KWENYE DRIVE



DONE

Hatua  hizi  unaweza  zifanya  kwa  mafaili  ya  aina  yote  utakayo  na  yanakua  salama so  hata  ikitokea  umepoteza  simu  yako  au umepoteza  hard copy  ya  vitu  vyako  bado  unakua  na  backup  ya  data  zako  muhimu  kwenye  DRIVE  bila  tatizo  lolote


MASWALI YANAYOWEZA KUULIZWA KWENYE INTERVIEW YA TRA MARCH 2025

  ANGALIZO Haya ni baadhi ya mawaswali  ambayo yanaweza yakatoka au yasitoke kutokana na ajira ulioiomba, hiyo unatakiwa kuyapitia na kuso...