“Unaweza kumnunua
binadamu
lakini
uwezi kummiliki binadamu”
“Umekuja
duniani peke yako,
na utaondoka peke
yako” hayo ndio
maneo nahisi wahenga
hawakupaswa kuyasema maana
watu wengi wanalia
kwa uwepo wake maishani
mwetu, ingawa ukiangalia
ni maneno yenye
ukweli, maana ulizaliwa
peke yako! lakini
njiani katika safari
yako ya maisha
ukakutana na mtu (someone
special) aliyebadilisha maisha
yako na kufanya
jambo moja zuri
au baya ambalo
ujawahi kulifanya maishani
mwako, UKAMPENDA, NDIO ukampenda
na kumpa moyo
wako na kumfanya
awe kila kitu
maishani mwako akakufanya
uingie kwenye ulimwengu
mpya, ulimwengu wa
mapenzi, ukamkabidhi moyo
wako na ukampa
pendo lako, ukashare
nae busu lako
la kwanza, mwili
wako kwa mara
ya kwanza. ukajiona
umebarikiwa kuliko wanawake/wanaume wote
duniani.
Muda ukapita
masaa, siku, wiki
miezi miaka mkawa
na furaha huku
ukiamini umempata wa kufa
na kuzikana nae (the one), na
ukaamini hakuna kitu
kingine ambacho ungemuomba
Mungu akupatie isipokuwa
muda wa furaha
ulionao na umpendae.
Kwakua amekamilisha maisha
yako
Lakini kila
mahusiano hayakosi kasoro,
kunakukwazana, kugombana na
muda mwingine hutumika
maneno ambayo hamkusudii kuyasema, lakini
kivyovyote vile hali
inavyokuwa! Mlitafuta njia
na kusameheana kama
vile wapenzi wa
kweli wafanyavyo kusuruhisha
matatizo yao na
kurudisha penzi lao
kwenye mstari. Lakini
yote hufanyika na
kuhesabika na mwisho
huchukuliwa kama malimbikizo
ya makosa ambayo
hutoa hukumu la
penzi lenu, kunasababu
nyingi za watu
kutengana kama vile kutovumilia
tabia
zisizo badilika, kufanya
kosa lisilosameheka, lengo
lake limetimia, kudanganyika na
watu wengine, kushidwa
kuvumilia hali ya
kiuchumi mlionayo, kupata mtu
mwingine, kuona
mpenzi wako hana
mipango ya baadae
na wewe, hakuna anachokipata
kwako, wazazi,
kuchokana, mpenzi
wako kutoendana na
hadhi uliyonayo, muda
aliyojiwekea kuwa kwenye
mahusiano na wewe
umeisha, na nk sababu
zipo nyingi mno.
Ila unachotakiwa ujue
ni kwamba sio
kila anaeingia kwenye
mahusiano anakuwa na
malengo ya dhati
na wewe, wewe
unaweza ukawa kwenye
mapenzi ila mwenzio
anapita tu kwa
muda, kivyovyote vile
inavyokuwa, bado kumpoteza
mtu umpendae INAUMA.
Sio wote
wanaoumia na mapenzi
wanamapenzi ya dhati,
wengine wanakuwa wamepoteza
mtu aliokuwa ni
msaada kwao. ila asikwambie mtu
hakuna kitu kinachouma zaidi ya
kumpoteza mtu umpendae,
na hapo ni
katika kutumia lugha
laini ila ukweli
ni kwamba hakuna
kitu kinacho uma
kama kuachwa au
kufikia maamuzi ya
kuacha. unajikuta umejaribu
kila kitu kufanya
mahusiano yaendelee lakini
mwisho wa yote
kunakuwa hakuna njia
nyingine zaidi ya
kuachana.
Watu wengi
hupitia wakati mgumu
baada ya kutengana
na wapenzi wao,
mawazo ndio pekee
yanayobaki kwenye kichwa
chako, utakumbuka kila
kitu mlichokuwa mnafanya
na kuomba umpendae
awepo mikononi mwako
wakati huu walau
umshike uhisi joto
lake la mwili
uone tabasam lake,
umkumbatie, umbusu na
kusikia yale maneno
matamu aliyokuwa akikwambia,
lakini inakuwa kama
ndoto, maaana unajikuta
kama unatoka usingizini
na kukutana na
maumivu ya moyo.
ukweli ni kwamba
tumeumbwa tofauti na
kila mtu ananjia
yake ya kukabiliana
na matatizo aliyonayo.
Kuna wale wanao
shindwa kukubaliana na
hali iliyotokea hivyo kushidwa
kuvumilia na kuamua
kuchukua maamuzi ya
kukurupuka na wengine
kuchukua maamuzi
ya kujiua au
kuhangaika wajuavyo ili
wawarudeshe wawapendao maishani
mwao, kuna wale
wanaoweka maumivu yao
moyoni na kubaki
wakiumia ndani kwa
ndani, kama nilivyosema!
kila mtu ananjia
yake ya kukabiliana.
Kama unataka kujua
jinsi ya kumsahau
mtu ulieachana nae
tafadhali fuata hizi
hatua nitakazo kuorodhesha
hapa chini.
MAMBO
YA KUFANYA
HATUA
YA KWANZA
PUMZIKA – jipe
muda wa kupumzika
usafishe kichwa chako
kwani ni hali
ya kawaida kwa
binadamu yeyote kuwa
kwenye maumivu uliyonayo.
Kumbuka wewe sio
wa kwanza na
hautakuwa wa mwisho
kukutana na jambo
kama hili. unatakiwa
kujua kuwa wapo
wengi waliopitia magumu
zaidi yako hivyo Usifanye maamuzi
ya haraka ambayo
yatakugharimu baadae. Usishindane
kuona wenzako wapo
kwenye mahusiano na
wewe ukaamua kurudi kichwa
kichwa, chukua muda
wa kutosha huku
unafanya mambo mengine.
Zitapita siku, wiki,
miezi hata miaka
lakini Mungu atakujalia
utampata atakaye kupenda
kwa dhati na
kukufanya usahau yote
yaliyopita.
HATUA
YA PILI
Jisamehe Usijilaumu - ingawa
nikawaida kurudisha mkanda
nyuma na kufikiri
sababu ya kipi
kichosababisha hadi ukaachana
na mpenzi wako,
na kujikuta ukijilaumu
kwa makosa uliyofanya
au muda ulioupoteza
kuwa naye. Utafikiria
mengi mitihani mliyopitia,
mambo mliyofanya, mambo
uliyomfanyia, ndoto zenu
mlizo panga,, ahadi
mlizowekeana na mendine
mengi. Utakosa majibu
lakini inakubidi ujisamehe
ili uweze kuendelea.
Jisamehee, Uache moyo
wako ukiwa huru.
HATUA
YA TATU
Msamehe – jambo la
msingi unalotakiwa kufahamu
ni kwamba daima
makovu yanatukumbusha tulipotoka
na watu walioyasababisha, hivyo
basi ili kuwa
na amani kwa
wakati ulionao na
wakati ujao hunabudi kumsamehe
mpenzi wako huyo wa
zamani ili kumtoa
akilini mwako, inakupasa
umsamehe kwani ukimchukia
utajipa mawazo ya
kumfikiria mara kwa
mara na kumuweka
kichwani huku ukiwaza
ya nyuma (would’ve, could’ve,
should’ve). Jambo ambalo
hastahili tena kwako.
HATUA
YA NNE
Ondoa
Uwepo Wake Katika
Maisha Yako Mapya. Unless
unatatoo yake mwilini
mwako!, Ila kwa
vitu vingine Unapaswa
kushugulikia kila kitu
kinacho kukumbusha mpenzi
wako wa zamani,
rudisha zawadi alizokupa,
kusanya vitu vyake
vyote ambavyo unavyo
viweke kwenye mfuko
au box kisha
mrudishie (kwakuwa uhitaji
kuonana nae inakupasa
umpe mtu ampelekee)
au weka stoo
au sehemu yoyote
ambapo hutaweza kuviona.
Futa picha au
ziweke kwenye kifaa ambacho
hutakuja kukitumia kwa
muda mrefu. Usitupe
na Usichome moto
au kuviharibu vitu
vyake uwezi jua
baadae vinaweza kuwa
na umuhimu wake
na utashukuru hukuvitupa.
Kuna
mazingira mengine yatashindikana kutoa
uwepo wake kwako, kwani
unaweza kuwa unasomanae,
mpo darasa moja (ni
group member mwenzako), mpo
ofisi moja, mnasali
kanisa moja. Anaweza
kuwa ni bosi
wako ambaye kila
siku unatakiwa umkabidhi
ripoti, au mfanyakazi mwenzako,
mwalimu wako na n.k ( hii
ni maada
ijayo utaipata kwenye
blog hii hii
kwenye machapisho yajayo
usikose, stay tuned)
b
HATUA
YA TANO
hBADILI MAZINGIRA (TAKE
A VACATION/ TRAVEL AND
CREATE NEW MEMORIES
DO SOMETHING AWESOME
AND LOCALLY AMAZING) - Kama
ratiba na hali
ya kiuchumi inakuruhusu
badili mazingira, ni
vizuri ukasafiri ili
kubadili mazingira na
kutengeneza kumbukumbu mpya, nenda sehemu
yeyote kama
mbuga za wanyama,
kawaone wazazi, mtembelee
rafiki yako kipenzi
aliyembali, nenda mji
ambao hujawai kufika
(tembelea sehemu za
makumbusho, nenda viwanja
vya mipira, tembelea
vibanda vya TV rufufu ila usiangalie pilau,
tembelea maktaba
zilizopo eneo hilo)
HATUA
YA SITA
Badili ratiba
yako ya maisha
ya kila siku – usitabirike, badili
ratiba yako siku. Hakuna
akujuae vizuri kama
mpenzi wako hivyo
ni wazi anajua
mwanzo mwisho ratiba
yako na inakuwa
rahisi kwake kujua
cha kufanya juu
yako au kukutafuta
atakapojisikia, kama ratiba
yako inajulikana kuwa
ukiamka asubuhi saa
4 unakwenda mgahawani
(your favourite dinner) Sio
kwa kumuogopa mtu
HATUA
YA SABA
BADILI MWONEKANO
WAKO.
Usionekane kama unamajonzi
au mfiwa, kuwa
smart, endelea kula
vizuri, vaa vizuri
tengeneza nywele zako
upatapo muda
HATUA YA NANE
TAFUTA MAHALI PA
KUWEKA UPENDO WAKO. Kwa
wale waliobarikiwa kuwa
na watoto (single
parents) inakuwa rahisi sana
kwao kwani wanaweza
kutumia muda wao
mwingi kuwa na
watoto wao na
kila maamuzi watayofanya
yatakuwa ni kwa
ajili ya manufa
ya watoto wao,
tumia muda wako
mwingi kuwa na
mwanao/wanao kwani ndio
watu muhimu uliobaki
nao, mtoto
wako ni rafiki
yako, ni kipenzi
chako. Kuwa mama/baba
bora kwa kuhakikisha
mwanao anapata malezi
bora usitetereke. Msaidie
homework, Toka out
katembee na mwanao
mpeleke sehemu za
makumbusho ,geuka uwe mtoto, ikikubidi
cheza nae gorori, rede
au mpira, weka
muda wa kukaa
nae chini uongee
nae.
Kama huna
mtoto tafuta paka
au mbwa. Ni
bora kuliko kukaa
peke yako
HATUA
YA TISA
PANGA MIPANGO YA
UCHUMI YA SASA
NA BAADAE ( PLAY THE
LONG GAME) -
ili usitetereke na
kuendelea kulaumu na
kumfikiria mpenzi wako
ndio sababu ya
kuanguka kwako inakubidi
uandae mipango endelevu ya
baadae ya maisha
yako, panga utakachofanya
kujiingizia hela sasa
na baadae, anzisha miradi
ya kukuingizia fedha
kila siku, anzisha miradi
itakayokuingizia hela baadae
usichague kazi. Kama
huna mtaji tafuta
ajira sehemu yeyote
usichague hata kama
mshahara ni mdogo
mradi utatosha kuweka
pesa kidogokidogo ya
kuanzisha kitu unachotaka
kufanya baadae.
HATUA
YA KUMI

HATUA
YA KUMI NA
MOJA
USALAMA
WA UNAPOISHI hakikisha
mahali unapo kaa kuna
usalama baada ya
kuchana mpenzi wako,
kama mlikua mnakaa pamoja
ni wazi atakua
anajua kila kitu
kuhusu nyumba yako
badili vitasa au
kufuri na uweke
vipya ili uwe na
amani.
MAMBO YA KUTOFANYA
USIJITENGE NA
WANAOKUJALI baadhi yetu
tumekosa bahati ya kuwa
na marafiki lakini
haimaanishi hatuna watu
wanaotujali, mwanzoni utapenda
kuwa peke yako,
utaona kila mtu
ni walewale lakini
sio sahihi, kuna
watu muhimu wanaokujali
na kukupenda na
daima watakuwa karibu
na wewe pale unapowahitaji, so
usijitenge nao kwani
ni moja ya
familia uliyobaki nayo.
USIGOMBANE NA WATU baada ya
kuachana na mpenzi
wako ni dhahiri
maneno mengi yataanza
kusemwa na kila
mtu ataongea lake
ili mradi tu.
USILIPIZE KISASI
iwe mmeachana kwa
heri au shari
jitahidi kutolipiza kisasi,
najua utakuwa na
hasira utafikiri mengi
unaweza ukawa umebaki
na picha za
utupu za mpenzi
wako au unajua
dili haramu alizopiga
zamani ili kumkomoa ukaamua
kuweka hadharani ili
umuharibie na aumie
kama unavyoumia wewe .
Jua kwamba kufanya
hivyo utakuwa umekosea
maana sio yeye
tu atakaye dharirika
ila na wewe
uliesababisha, na watu
watakushusha hadhi yako
na kukudharau kwa
kitendo ulichokifanya hata
bila ya hayo
nafsi yako itakusuta
baadae na unaweza
juta kwanini ulifanya
hivyo ndio maana
wanasema hasira hasara.
USITOE SABABU ZA
KUACHANA KWENU KWA WATU
BAKI – kuachana na mpenzi
wako isiwe faida
kwa watu wengine,
jitahidi kutosema ovyo
kwa watu sababu
za kuachana kwenu.
kumwambia rafiki mmoja
au wawili unaowaamini
inatosha
EPUKA KWENDA
MAENEO YATAKAYO KUFANYA
UMKUMBUKE Kumbukumbu ndogo
ndogo zinafanya tuendelee
kuwashikilia watu tuliotengana
nao, kila kitu
kina kumbukumbu zake
kuanzia nguo tunazovaa,
vijiko tunavyotumia, nyimbo
tunazo sikia, movie
tunazo angalia, makochi
tunayokalia, vitanda tunavyolalia
na pamoja na
sehemu mbalimbali tunazotembelea Jitahidi kutokwenda
maeneo ambayo yatakukumbusha mpenzi
wako wa zamani,
kunauwezekano mlipenda kutoka
kila weekend na
kwenda maeneo mbalimbali
na mpenzi wako
huyo, club, bar
dinner, beach, guest
na nk.
EPUKA ULEVI: Muhudumu
Ongeza Glass ndio wimbo
wa taifa, pia
hutumika na watu kama
wewe
mliotendwa na wapenzi wenu. Jambo
la
mwisho unalotakiwa kufanya
ni kunywa pombe,
na kuonekana chizi
mbele ya macho
ya watu. Ndio umeachana
na mpenzi wako
ila hiyo isiwe
sababu ya wewe
kuharibu maisha yako,
tabia inajenga mazoea,
utakapoanza ulevi ni
dhahiri utaendelea kuwa
mlevi, maana pombe
itakuongezea mawazo na
sio kupunguza pia
utashusha naendeleo yako
kwani pesa zako
zote zitaishia kwenye
pombe.
EPUKA MARAFIKI
ZAKE kama ulipata
bahati ya kutambulishwa
kwa wazazi na
marafiki wa mpenzi
wako wa zamani
inamaanisha na yeye
alikupenda pia, ila
mambo yamebadilika na
imekubidi mtengane cha
kufanya wakati upo
kwenye majonzi ni
kukaa mbali na
marafiki zake ili kuepusha maswali
na kusikia habari
zake.
MITANDAO YA
KIJAMII jitahidi kuepuka mitandao
ya kijamii, jua
kuwa upo katika
muda wa kujiweka
sawa na kitu
cha mwisho unacho hitaji
kwa sasa ni
kukutana na habari
zitakazo kutia simanzi au kuona
picha ya mpenzi
wako wa zamani
akiwa na furaha
na mtu mwingine.
Vile vile inakubidi
kuepuka usumbufu wa
watu wengine, Kumbuka
uliposumbuliwa pindi upo
kwenye mitandao ya
kijamii (hasa pale
statues zako zilivyokuwa
single) sasa kurudi
tena ni kama
swala kukatiza katika
msitu wa simba au
mbwa mwitu, bora
simba unaweza kukutana
nae mmoja akakufaidi
peke yake, ila
mbwa mwitu wanatabia
ya kutembea kikundi
na ukipita anga
zao kila mmoja
ataondoka na kipande
chake.
USIKUBARI KUWA NA
URAFIKI NAE
MAPEMA ni jambo
la kwaida kuendelea
kuwa na mahusiano
ya kirafiki na mtu ambaye
alikuwa ni mpenzi
wako zamani, ila
inakubidi ujaribu kuepukana
naye kipindi cha
mwanzoni baada ya
kuachana kwenu na
kama yeye anakujali
hatakusumbua
USIBADILI TABIA
YAKO kitu kimoja inakupasa
ukitambue, usiruhusu mtu
akubadilishe ulivyo kwa
ajili ya furaha
yake. ni dhairi utakuwa
umechanganyikiwa baada ya kuachana na
mpenzi wako, utajaribu
kila njia ya
kumsahau katika hatua
hizo kunauwezekano ukabadilika
na kujipoteza, nafsi
yako iliyozoeleka ikaondoka
na watu wanakujali
wakaona mabadiliko ambayo
hawakujazoea, mf utabadili
tabia utakuwa mtu
wa hasira na
matusi wakati ulikuwa
mpole, ulikuwa unakwenda
kuabudu kanisani au
msikitini utakuwa mtu
wa viwanja. Usijione
kwamba unamapungufu ndio
maana mahusiano yenu
yamevunjika, jua kuwa
mpenzi wako alikupenda
kwa tabia yako,
tabia uliyokuwa nayo
kabla ujakutana naye
may be ilikua nzuri
au mbaya ila
kama familia yako
walikusifu basi haupaswi
kuibadili.
KUANZISHA MAHUSIANO
MAPYA ILI KUMFANYA
X
AWE NA WIVU
JUU YAKO – epuka kuanzisha
mahusiano mapya mapema
na watu wengine
kwa lengo la
kumfanya mpenzi wako
awe na wivu,
unaweza ongeza tatizo
baada ya kupunguza,
vilevile unaweza kumuumiza
mtu unayemtumia kwani
naye anaweza kuwa
na mapenzi ya
dhati juu yako. Vile
vile itashusha thamani
yako.
USIBEMBELEZE
- Kunauwezekano makosa
yalikuwa yako au
yake ila kabla
ya kuachana kwenu
ulijitahidi kufanya kila
kinachowezekana kuhakikisha mmbo
yenu hayazidi kuwa
mabaya, ukatafuta wasuruhishi
ukabembeleza, na
kubembeleza, na kuzidi
kubembeleza, lakini jitihada
zako hazikuzaa matunda.
Nakushauri usiendelee kubembeleza
tena baada ya
kuachana, maana kufanya
hivyo utakuwa mtumwa
na utaendelea kujidharirisha na
kushusha hadhi yako
zaidi na kumpa
kichwa mpenzi wako
na atakuona kuwa
huwezi kuendelea bila
yeye, na utakuwa
unamkufuru Mungu. Inakubidi
utambue kuwa ulifanya
kila kinachowezekana lakini
ikashindikana.
USITIE HURUMA – usiwe katika
hali ya kuwa
mnyonge kupitiliza ili
watu wakuone na kuamini
watapeleka ujumbe kwa
mpenzi wako ili mrudiane. Jua
swala hilo linaweza
kufanya kazi au
likafeli na kujikuta
unaendelea kujidharirisha tu
mbele yake na
kwa watu wakuzungukao.
TOA MATUMAINI
YA KURUDIANA NAE
usiwe na imani
ya kwamba aendapo
atakosa mtu mwingine
atakayempenda kama wewe
ulivyo mpenda au
yatamkuta mabaya na
atarudi tena kwako.
Jua kuwa Uwezekano
huo upo na
uwezekano huo haupo
maana “dua la
kuku halimpati mwewe”.
Kuwa na imani
hiyo kutakufanya wewe
usiendelee na maisha
yako huku muda
ukienda, mwenzio atapata
mtu mwingine atakaye
mpenda zaidi yako, ataanzisha familia,
hata kama itatokea
akaachana nae kunauwezekano
asirudi kwako atatafuta
mtu mwingine wakati
huku wewe ukiendelea
kusubiri. Na kama
atarudi, atarudi kipindi
amechoka, katumiwa hadi
kaisha hana mtu
mwingine anaye mtaka
ndio anarudi kwako
(nikawaida ya binadamu,
tunapopata matatizo tunakumbuka
tulipotoka na watu
waliokuwa wanatujali kipindi
hatuna kitu, baada
ya kupata tunasahau
yote na kuwaacha
wapendwa wao nyuma)
Unachotakiwa kufanya fanya
mambo yako akitokea
mtu atakaye dhihirisha
upendo wake kwako
fungua moyo wako
mpende usimfananishe na
mpenzi wako wa
zamani jua kuwa umeanza
ukrasa mpya (I
know how it
feels, I know
its hard to
fall in love again
for people who
truly loved once.
Someone will come
around , when then
do …. don’t replace them,
just start over)
lakini hakikisha umesamehe
na usiwe na
imani ya kurudiana
ila muombee apate
mtu atakaye mpenda
na kumthamini zaidi
ya wewe ulivyompenda
na kumthamini fanya
hivyo ili baadae
asije kukusumbua na
kukukumbusha machungu uliyoyasahau.
MAMBO YA KUJIANDAA
MASWALI -
marafiki wataona mabadiliko
pamoja na wanafki
pia, wote wanojua
na wasiojua watakuuliza
maswali ili kujua
kwa undani sababu
za kutengana kwenu.
Hivyo unatakiwa kujiandaa na
maswali hayo. Kweli hayawahusu
ila hutakiwi kuonesha
hasira.
KUKUTANA NAE:
milima haikutani binadamu
wanakutana, baada ya
kuachana jua kwamba
ipo siku unaweza
kukutana na mpenzi
wako wa zamani.
Usioneshe kukasirika ukionana
nae itikia salamu
kama atakusalimia kisha
endelea na mambo
yako, hakuna haya
ya kupeana namba
au kujua nini
unachofanya. Kumbuka hujabadilika,
wewe ni Yule Yule alie
kuacha na ni Yule
Yule anaekuona
wa maana sasa.
KUTAFUTWA baada
ya kuachana na
mpenzi wako jua
kwamba mbele ya
safari lazima atakutafuta, usishangae
kuona friend request kwenye FB au namba
ngeni inakupigia na
kujitambulisha kuwa yeye
ni x wako,
KUTONGOZWA, ulipokuwa
kwenye mahusiano watu
walikutaka na unapotoka
kwenye mahusiano usishangae
hata mashemeji zako
wakaomba mzigo, ndio! Hilo
ndio
neon linalotumika kwa
sasa.
KUTISHWA, muda utapita
na wewe utaendelea
na maisha yako,
ila baadae mpenzi
wako anaweza kutaka
kurudiana na wewe, anajua udhaifu
wako ataanza kwa
upole na kukukumbusha
mambo ya nyuma
na jinsi mlivyokuwa
na furaha utakapo
mkatalia usishangae kupata
vitisho toka kwake.
MAMBO YA
KUKABILIANA NAYO
UPWEKE – kuna uwezekano mkubwa
ukawa pekeyako katika kipindi
hicho chote , ulishazoea
kulala na mpenzi
wako sasa upo
pekeyako kitandani, unamiss hata
mabishano mliokuwa mnabishana. Usijali! Itakuwa
vigumu mwanzoni lakini
badae utazoea na
utakuwa sawa

Cha kuzingatia:.
Mara nyingi
inapotokea jambo kama
hili la kutedwa
watu wengi hutupia
lawama kwa jamii
ya mtu aliemtenda.
Mf wanaume huwaita
wanawake Malaya kwasababu
tu aliachwa au
alimuacha mwanamke aliymkosea.
wanawake nao hivyo
hivyo huwaita wanaume
walewale kwasababu ya
kutendwa na mtu
mmoja. Kiukweli jambo
hili sio sawa,
sababu zinazofanya uchukue
imani hizo ni
kwamba baada ya kutendwa
ulikurupuka bila kupumzika
na kuanza mausiano
mapya na watu
wengine bila kufikiria
ili tu uweze
kupunguza maumivu uliokuwa
nayo, kuogopa upweke au
ulitaka kulipiza kisasi
kwa kutembea na
rafiki yake au
akuone utetereki kwa
kuwa upo na
mtu mwingine (kata mti
panda mti, ukishuka wenzio
wanapanda, ukisema cha
nini …….. na nk), hata
hivyo mtu huyo
uliekuwa unamtumia hukuweza
kuendelea nae kwakuwa
ulijilazimisha kuwa naye.
kama nilivyosema
mwanzo sio kila
mtu anaeingia kwenye
mahusiano anakuwa na
malengo ya dhati
sio kwamba kila
anaeingia kwenye mahusiano
anamalengo mabaya, mapenzi
ya mapenzi ya
kweli yapo
Muda utapita vidonda
vitapona, utasahau
Atatokea
mwingine anaweza kuwa
mbaya kuliko mpenzi wako
wa zamani
Au anaweza kuwa
bora zaidi ya mpenzi
wako wa zamani
Maisha yanaendelea
USIPANGE KUWA
NA MALAIKA. Jua
kabisa hali hii haitakuwa
ya kudumu ipo
siku utapata mtu
mwingine. Tatizo tulilonalo
binadamu ni kwamba
ikitokea mtu amepatwa
na mkasa kama
huu atajitahidi kutafuta
mtu ambaye ni mzuri zaidi
ya Yule aliyeachana
nae. Jambo ambalo
litakufanya uendelee kutumika
maana utategemea kuwa
umepata malaika
kumbe umeangukia mikononi
mwa shetani matokeo
yake ni moto
kila siku ndani
Next topic
HOW DO TO
FIND TRUE LOVE
Mapenzi ya kweli
hayachagui,
Awe mzuri, mbaya, hana elimu lakini ana mapenzi
ya kweli. je utamkataa kwasabau Hana cha kukupa zaidi ya mapenzi aliyonayo. Haijalishi
watu wengine wanamuonaje
(marafiki/ wazazi)
kinachojalisha ni furaha
yako wewe na
yeye. Muda ukifika
wataelewa.
Jina langu ni Ago, kutoka Albania. Nitapenda kushiriki uzoefu wangu juu ya jinsi ninavyopona mpenzi wangu mzuri kutoka kwa mnyang'anyi wa mke
ReplyDeleteNilipoteza rafiki yangu wa kike safi na mzuri kwa mtu mwingine. Nilikuwa na huzuni na nilitaka arudi vibaya tena. Nilikuwa nikimpigia Dk.Sango kwa usomaji na ushauri na nikagundua atanisaidia. Uchawi wake wa upatanisho ulimrudisha mpenzi wangu mpendwa. alisahau kabisa juu ya yule mtu mwingine na alirudi kwangu akiwa wazi na mwenye upendo kama hapo awali. Sasa wasiliana na daktari, Dk Sango, ikiwa unahitaji kushauri juu ya uhusiano wako au aina yoyote ya shida kwenye barua pepe yake. inaelezea mtaalam937@gmail.com
Nilikuwa kwenye hatihati ya kumpoteza mke wangu wa miaka sita kwa sababu alisema hakuwa na hamu tena na ndoa yetu, ambayo inalea binti mzuri kwa sababu kama dereva wa lori huwa nikienda barabarani, lakini nampenda sana na namjali mke wangu. Nilimuuliza yeye na binti yangu shida ni nini, lakini hakutoa ufafanuzi mzuri, akisema alikuwa amechoka na umoja wetu, ilikuwa ya ajabu kwangu kwa sababu mke wangu alikuwa mwanamke mwenye upendo, ghafla kila kitu hubadilika tu. na mtazamo wake kwangu haukuwa mzuri, nilijua ilikuwa mbaya mahali pengine, kwa hivyo nilielezea mambo kwa rafiki yangu mzuri Micheal, ambaye alinitambulisha kwa jina la mwandishi wa spell Dr.Pellar, nilielezea hali yangu kwa mwandishi, ilifanya ninatambua kuwa mpenzi wa zamani alikuwa akimdanganya mke wangu kuniacha, lakini akaniambia nisiwe na wasiwasi. Nilifuata maagizo yote na mke wangu alirudi kwa ustawi wake wa kawaida na ninashukuru sana kwa kile msaidizi wa Dr.Pellar amenifanyia, kwa hivyo nashiriki shuhuda zangu ikiwa unakabiliwa na shida yoyote maishani na unahitaji suluhisho kuwasiliana na daktari huko DrPellar kwenye barua pepe yake drpelar@gmail.com
ReplyDeleteNilikuwa kwenye hatihati ya kumpoteza mke wangu wa miaka sita kwa sababu alisema hakuwa na hamu tena na ndoa yetu, ambayo inalea binti mzuri kwa sababu kama dereva wa lori huwa nikienda barabarani, lakini nampenda sana na namjali mke wangu. Nilimuuliza yeye na binti yangu shida ni nini, lakini hakutoa ufafanuzi mzuri, akisema alikuwa amechoka na umoja wetu, ilikuwa ya ajabu kwangu kwa sababu mke wangu alikuwa mwanamke mwenye upendo, ghafla kila kitu hubadilika tu. na mtazamo wake kwangu haukuwa mzuri, nilijua ilikuwa mbaya mahali pengine, kwa hivyo nilielezea mambo kwa rafiki yangu mzuri Micheal, ambaye alinitambulisha kwa jina la mwandishi wa spell Dr.Pellar, nilielezea hali yangu kwa mwandishi, ilifanya ninatambua kuwa mpenzi wa zamani alikuwa akimdanganya mke wangu kuniacha, lakini akaniambia nisiwe na wasiwasi. Nilifuata maagizo yote na mke wangu alirudi kwa ustawi wake wa kawaida na ninafurahi sana kwa kile msaidizi wa DrPellar amenifanyia, kwa hivyo nashiriki shuhuda zangu ikiwa unakabiliwa na shida yoyote maishani na unahitaji suluhisho kuwasiliana na daktari huko DrPellar kwenye barua pepe yake drpellar@gmail.com
ReplyDelete